.

Wadau wa CHF

Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Uanzishwaji wa Wizara ya Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa imetajwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 8 (1) 145 na 146 ya 1977 na marekebisho mengine mengi yaliyofuata. Mwaka wa 1982 chini ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Mamlaka za Serikali za mitaa No 7 (Cap 287) na Sheria ya Mamlaka za Mjini No 8 (Cap 288). Sheria hizi mbili zilitoa mamlaka kwa Waziri mwenyedhamana na tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa juu ya uanzishwaji wa Mamlaka za serikali za Wilaya, Vijiji, Miji midogo, pamoja na Mitaa. 

www.tamisemi.go.tz


Wizara ya Afya

Malengo mahsusi ya wizara hii ni kuhakikisha kuwa inatoa huduma za msingi ambazo ni nzuri, zenye ubora, ulinganifu, zinazopatikana, bei rahisi, zinazodumu na zinajali masuala ya jinsia. Hatima ya yote hayo ni kuwa na jamii yenye afya bora itakayoweza kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. 

www.moh.go.tz


HPSS Tuimarishe Afya

Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya unapambana kuhakikisha ya kuwa unaboresha ubora wa upatikanaji wa huduma za afya katika mikoa yote ya Tanzania. Lengo la mradi ni kuboresha hali ya afya na ustawi wa maisha ya watanzania, juhudi zaidi zikiwahusu watu walio katika hatari zaidi na kuiwezesha sekta ya afya kukabiliana na mahitaji yote ya afya kwa watu wote nchini. Lengo la mradi likiwa ni kuboresha ubora, upatikanaji, na utumiaji wa rasilimali na huduma; na kuona hizi huduma zinatolewa na mfumo wa afya ulio bora. 

www.hpss.or.tz


The Swiss Tropical and Public Health Institute (Swiss TPH)

Mradi wa Swiss TPH ni miongoni mwa miradi inayo ongoza duniani katika utafiti wa masuala ya afya, mafunzo na utoaji wa huduma. Inaboresha, inadumisha na inakuza afya ya mtu mmoja mmoja na afya za jamii duniani kote. Mkazo ukiwekwa katika nchi ambazo zinakabiliwa na uchache wa rasilimali. Mradi huu unatoa huduma mbalimbali ikiwemo masomo ya maabara, kazi za kliniki, na uhamishaji wa vitendo wa dhana na utaalam wa kiufundi katika kupanga na mipango ya sekta ya afya. Ushirikishaji na kujifunza kwa pamoja ndiyo msingi wa mafanikio yetu. 

www.swisstph.ch


The Swiss Agency for Development and Cooperation (SDC)

Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi, ni sehemu ya Ubalozi wa Serikali ya Uswisi nchini Tanzania. Unawajibu wa kutekeleza sera za Baraza la Shirikisho la Sera za Nje ya Serikali ya Uswisi katika masuala ya misaada ya kibinadamu, ushrikiano wa maendeleo na ushirikiano na Ulaya Mashariki.  Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi linasaidia nchi ambazo zipo katika jitihada za kujikomboa kutoka katika umasikini na changamoto za maendeleo. Haswa, linasaidi makundi yenye shida mbalimbali katika jamii kupata elimu, afya na kutatua changamoto za mazingira. Usawa wa jinsia na utawala bora ni misingi inayo liongoza Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi. 

www.eda.admin.ch/sdc


PharmAccess

PharmAccess ina amini katika kuboresha huduma za afya. Ikiwa na mkazo wa shughuli zake Kusini mwa Sahara, Mradi wa Pharmaccess unafanya kazi katika kuimarisha mfumo wa afya. Hivyo basi, inafanya hivyo kwa kukusanya rasilimali za umma na binafsi ili kupata fedha zitakazo weshesha kuboresha mfumo, kupima na kuboresha ubora na kuwafikia wale walio sahaulika kupitia teknolojia rahisi kama za simu ya kiganjani. Huu mfumo wa afya umeandaliwa kuhakikisha kwamba kila mtu anafikiwa na huduma zilizo bora wakati wowote anapo zihitaji na sio tu wakati wanao uwezo wa kuzilipia.

www.pharmaccess.org