Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Ilianzishwa) na Serikali kwa sheria ya mwaka 2001; ambapo kila Halmashauri ilitakiwa kuanzisha Mfuko wa CHF. Tathmini ya uendeshaji wa mfuko huu imeonesha kwamba utekelezaji wake unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatokana na matatizo ya muundo na mfumo wa uendeshaji wake; matokeo yake kumekuwa na mafanikio tofauti baina ya Halmashauri moja na nyingine.
Kufuatia changamoto hizo Serikali imedhamiria kufanya maboresho katika maeneo matatu ili kuimarisha uendeshaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii.Maeneo hayo ni;Usimamizi na Uendeshaji (Governance),Usajili wa wanachama wa Mfuko (Enrolment), Kitita cha mafao na ngazi ya upatikanaji wa huduma za Afya (Benefit Package).
Soma zaidi
Mwanachama wa CHF atapata huduma zote za matibabu kwa kufuata utaratibu wa rufaa kwa ngazi zote za vituo vya kutolea huduma vya serikali.
Kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii ( CHF Iliyoboreshwa) tembelea Ofisi ya Mtaa / Kijiji kwa Afisa Mwandikishaji au kwa wakala aliye idhinishwa, utafamyiwa usajili wa kaya kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ya simu ya mkononi. Ambapo kila mwanachama atapigwa picha bure na kupewa kitambulisho.
Pia kwa mwanachama aliyefikia kikomo cha Uanachama wake utahuishwa kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ya simu ya mkononi.