.

Maswali ya mara kwa mara

Ni Bima ya Afya Jamii ambayo inamilikiwa na Serikali ya Tanzania chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI), ambapo familia isiyozidi watu sita husajiliwa kupitia Afisa Mwandikishaji katika Kijiji au Mtaa wako.

Ghrama ya malipo ili uwe mwanachama wa CHF Iliyoboreshwa ni shilingi 30,000/= kwa kaya ya watu wasiozidi 6; na kwa mkoa wa Dar es Salaam ni shilingi 40,000/= kwa mtu mmoja na shilingi 150,000/= kwa kaya ya watu wasiozidi 6.

CHF Iliyoboreshwa inatoa kadi kwa kila mwanachama ili kurahisisha kupata matibu popote unapohitaji matibabu.

Kuwa mwanachama wa CHF Iliyoboreshwa kunakupatia nafasi ya kujiandaa na usalama dhidi ya gharama gharama kubwa kabla ya kuugua. Mwanachama analipa gharama ndogo kipindi ambacho ana hela na inamfanya asiwe na wasiwasi wa kuuguza mwaka mzima kwa familia yake. CHF Iliyoboreshwa inakuwezesha kupata huduma katika vituo vya kutolea huduma vya serikali kuanzia ngazi ya Zahanati, vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na Hospitali za Rufaa za Mikoa.

Kupitia Mfuko wa Bima ya Afya, huduma zinazotolewa ni zile zote zinazopatikana katika Zahanati za Serikali, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, na Hospitali za Rufaa za Mikoa.

Mwananchama wa CHF Iliyoboreshwa anaweza kupata huduma za matibabu katika vituo vyote vya kutolea huduma vya Serikali nchini Tanzania Bara.

Kila mwananchi aliye nchini anaweza kuwa mwananchama wa CHF Iliyoboreshwa na kunufaika na huduma zote zitolewazo na mfuko huo. Mara baada ya malipo kufanyika mwananchama anaweza kupata huduma kwa kipindi cha mwaka mmoja. Utahitajika kuhuishwa uananchama baada ya mwaka mmoja ili kuendelea kupata huduma.

Unaweza kujiandikisha Bima ya Afya Jamii kupitia Afisa Mwandikishaji katika kijiji chako au mtaa wako. Pia unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti wa Kijiji au Mtaa ili kuweza kupata taarifa za muandikishaji.

Unaweza kuhuisha uanachama wako kupitia Afisa Mwandikishaji. Na pia waweza kuhuisha uanachama wako kwa kulipia kiasi kianachohitaji kupitia simu yako ya kiganjani na mfumo wa uandikishaji utakuhuisha. Piga namba *152*00# halafu chagua 2 (Afya), halafu chagua 5 (CHF).

Hapana, huhitaji kadi mpya baada ya kuhuisha uanachama wako. Kila mwanachama anatakiwa atunze kadi yake ya uanachama baada ya kuhuisha. Taafira za kuhuisha kwa mwaka unaofuta zitaingizwa kwenye mfumo na kadi yako itaendelea kutumika wakati wa kupata huduma.

Unaweza kutoa taarifa ya vitu vinavyo kutatiza kwa Mratibu wa CHF wa Halimashauri au kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji au Afisa Mtendaji wa Kata au Diwani au Mganga Mkuu wa Wilaya. Katika ngazi ya mkoa wasiliana na Mratibu wa CHF wa Mkoa au Mganga Mkuu wa Mkoa. Pia namba za mkoa wako utazipata hapa.

Tumia simu ya mkononi yenye mfumo maalum wa kusimamia madai au mfumo wa madai wa kimtandao kila siku. Wahusika wanazo akaunti maalum kuweza kuchakata malipo.

Utaratibu wa rufaa unasimamiwa kwa kujaza fomu za rufaa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za juu zaidi ya ngazi ya kutolea huduma. Baada ya kujaza fomu, mgonjwa ataiwakilisha katika ngazi ya juu ya kutolea huduma na taratibu za matibabu zitafuata.

Malalamiko na maswali kuhusu uandikishwaji yapeleke kwa timu za CHF Kata na Wilaya. Malalamiko kuhusu huduma za afya, uhaba wa dawa, miundombinu mibovu, wasiliana na Msimamizi wa kituo cha kutolea huduma au kwa Mganga wa Wilaya au kwa Mganga mkuu wa Mkoa. Kwa malalamiko na maswali ya ujumlawasiliana na Maafisa Ustawi wa Jamii, Ofisi za Wakurugenzi Watendaji wa Halimashauri na Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa.

Chukua ripoti ya upotevu toka Kituo cha Polisi kilicho karibu nawe au chukua taarifa ya upotevo toka Ofisi ya mtendaji wa Kijiji halafu ipeleke kwa Afisa Muandikishaji ambaye ataiwakilisha kwa Wasimamizi wake kwa michakato ya kupata kitambulisho kipya.