.

Huduma na Faida za CHF Iliyoboreshwa

Mwanachama wa CHF atapata huduma zote za matibabu kwa kufuata utaratibu wa rufaa kwa ngazi zote za vituo vya kutolea huduma vya serikali.

Huduma ngazi ya Zahanati
 • Ushauri wa daktari
 • Vipimo vya maabara
 • Vipimo vya picha ( X-ray na ultra sound)
 • Dawa
 • Uangalizi (Mapumziko)
Huduma ngazi ya Kituo cha Afya
 • Ushauri wa daktari
 • Vipimo vya maabara
 • Vipimo vya picha ( X-ray na ultra sound)
 • Dawa
 • Kulazwa
 • Upasuaji ( wa Kawaida na Mdogo)
Huduma ngazi ya Hospitali ya Wilaya
 • Ushauri wa daktari 
 • Vipimo vya maabara
 • Vipimo  vya picha ( X-ray na ultra sound)
 • Dawa
 • Kulazwa
 • Upasuaji ( wa Kawaida, Mdogo na Mkubwa)
Huduma ngazi ya Hospitali ya Mkoa
 • * Ushauri wa daktari 
 • * Vipimo vya maabara
 • Vipimo  vya picha ( X-ray na ultra sound)
 • Dawa
 • Kulazwa
 • Upasuaji ( wa Kawaida, Mdogo na Mkubwa)
 • Huduma za rufaa zilizopo ngazi ya mkoa
Huduma zisizogharamiwa na CHF
 • Huduma za kufunga viungo bandia, vya mwili, miwani, visaidizi vya sikio,visaidizi vya moyo
 • Vipimo vya MRI,CT scan, DNA typing
 • Operesheni kubwa kama za moyo, ubongo,figo n.k
 • Huduma za kuhudumia mwili wa marehemu
 • Huduma za kurekebisha mwili (cosmetic surgery)
 • Majeraha yanayotokana na nia ya mtu kujidhuru kama matumizi ya vilevi, utoaji mimba au kujaribu kujiua.
 • Matibabu kwa wajeruhi walioshiriki maasi kama vurugu,maandamano n.k
 • Kulaza kwenye ward za binafsi (private wards)
CHF Iliyoboreshwa